Senegal yapata ubingwa wa Kombe la 33 la Mataifa ya Afrika (AFCON)
2022-02-07 09:31:29| cri

Senegal yapata ubingwa wa Kombe la 33 la Mataifa ya Afrika (AFCON)_fororder_非洲杯

Fainali za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) imefanyika jana usiku nchini Cameroon.

Baada ya mchezo wa dakika 90 na dakika za nyongeza, Senegal na Misri zilitoka sare ya 0-0, na kulazimika kupigiana mikwaju, ambapo Senegal ikaitoa Misri kwa mikwaju 4 kwa 2 na kupata ubingwa kwa mara ya kwanza kwenye michezo ya AFCON.

Hii ni mara ya tatu kwa Senegal kuingia kwenye hatua ya fainali, ambapo mara ya kwanza ilikuwa 2002, na baadaye ni 2019, na zote ilichukua nafasi ya pili, huku Misri ikiwa ni mara yake ya kumi kuingia hatua ya fainali, ambapo ilichukua ubingwa mara saba katika fainali tisa, na Misri imekuwa nchi iliyopata ubingwa mara nyingi zaidi katika michuano ya AFCON.

Kutokana na janga la Corona, mwezi wa sita mwaka 2020 Shirikisho la Soka la Afrika lilitangaza kuahirisha michuano hiyo ambayo awali ilipangwa kufanyika 2021 nchini Cameroon hadi 2022.