Marais wa Misri na Djibouti wajadiliana masuala ya uhusiano wa pande mbili na ya kikanda
2022-02-08 09:41:54| CRI

Rais Abdel-Fattah al-Sisi wa Misri jana alizungumza na mwenzake wa Djibouti Ismail Omar Guelleh aliyeko ziarani nchini Misri juu ya masuala ya uhusiano wa pande mbili na ya kikanda.

Kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika mjini Cairo, rais Sisi amesema ziara ya Guelleh ni muendelezo wa mawasiliano na uratibu kati ya pande hizo mbili kwa ngazi mbalimbali, pia ni hatua mpya ya matokeo ya mashauriano yao wakati Sisi alipofanya ziara nchini Djibouti mwezi Mei mwaka jana. Shughuli hizi zinaonyesha uhusiano wa kimkakati wa muda mrefu unaoziunganisha nchi hizo mbili.

Rais al-Sisi ameongeza kuwa wamezungumza mambo ya ushirikiano unaoendelea, hasa kwa sekta za uchumi, biashara na uwekezaji. Pia wamebadilishana maoni juu ya ushirikiano kwenye sekta za elimu na afya.