Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Iran wafanya mazungumzo
2022-02-08 09:46:42| CRI

Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Iran wafanya mazungumzo_fororder_伊

Waziri wa Mambo ya Nje Bw. Wang Yi amefanya mazungumzo na mwenzake wa Iran Bw. Hossein Amir Abdollahian.

Bw. Amir Abdollahian alitoa pongezi kwa sherehe nzuri za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing na kusema kuwa michezo hiyo itakuwa ya mafanikio. Akitoa salamu za mwaka mpya wa jadi wa China kwa watu wa China, alisisitiza kuwa Iran inapenda kudumisha mawasiliano ya karibu zaidi na China katika nyanja zote ili kuzidisha ushirikiano wa kimkakati wa kina kati ya Iran na China.

Naye Bw. Wang Yi amesema China itaendelea kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana katika nyanja mbalimbali kati ya nchi hizo mbili, kuimarisha mawasiliano na uratibu na Iran katika masuala ya kimataifa na kikanda, na kukuza ushirikiano wao wa kimkakati wa pande zote.

Amir Abdollahian pia alimwelezea Wang kuhusu maendeleo ya hivi karibuni kuhusu mazungumzo ya kurejesha tena makubaliano yajulikanayo kama (JCPOA).

Amesema Iran imejitolea kwa dhati kufikia makubaliano hayo kwa njia ya mazungumzo huku ikiyalinda vyema maslahi ya taifa la Iran.

Wang amesema China inapongeza msimamo wenye kanuni wa Iran wa kusuluhisha suala hilo kwa mazungumzo na kuiunga mkono Iran katika kuibua madai yanayofaa wakati wa mazungumzo hayo.