UM yasema ukame mkali umeathiri watu milioni 4.3 nchini Somalia
2022-02-08 09:45:27| CRI

UM yasema ukame mkali umeathiri watu milioni 4.3 nchini Somalia_fororder_索马里

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Mambo ya Kibinadamu UNOCHA imesema, takriban watu milioni 4.3 wameathiriwa na ukame mkali katika baadhi ya sehemu nchini Somalia, kutoka milioni 3.2 mwezi uliopita.

Ofisi hiyo imesema ukame unaoendelea umesababisha takriban watu laki 2.7 kuacha makazi yao ili kutafuta maji, chakula na malisho.

Pia imesema Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kukabiliana na Dharura umetenga dola za kimarekani milioni 25 kwa ajili ya kukabiliana na ukame na Mfuko wa Kibinadamu wa Somalia umekamilisha ufadhili huu kwa kutenga dola za kimarekani milioni 6, huku mgawo wa pili ukiendelea. Fedha za ziada kwa sekta zinazopewa kipaumbele zinahitajika haraka ili kuokoa maisha ya watu, ikiwa ni pamoja na ufadhili wa Mpango wa Mwitikio wa Kibinadamu wa Somalia wa mwaka 2022.