Tanzania kuwapatia mafunzo ya kilimo cha kisasa zaidi ya wahitimu 12,000 wa vyuo vikuu
2022-02-08 09:43:02| CRI

Mamlaka za Tanzania zimesema Jumatatu kuwa zimewapatia mafunzo ya kilimo cha kisasa zaidi ya wahitimu 12,000 wa vyuo vikuu, zikiwa kwenye hatua inayolenga kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira.

Akijibu swali la mbunge wa viti maalumu Thea Ntara mjini Dodoma, aliyeitaka serikali ifafanue inafanya nini ili kutatua suala la ukosefu wa ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu ambalo linaikabili nchi hiyo, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana na Ajira Patrobas Katambi amesema kilimo cha kisasa kinaweza kupunguza idadi inayoongezeka ya vijana wahitimu wasiokuwa na ajira nchini na kwamba mbali na kuwapatia mafunzo ya kilimo cha kisasa, idadi kubwa ya wahitimu hao pia imenufaika na mafunzo ya stadi za kazi ambayo yatawasaidia kushindana vizuri kwenye soko la ajira.

Mbunge Thea ameona kwamba maelfu ya wahitimu wa vyuo vikuu wamezagaa mitaani, wakiwa hawana kazi wakati nchi ina ardhi kubwa ya kilimo lakini changamoto kubwa ni kwamba hawana ujuzi wa kufanya kazi kwenye sekta ya kilimo.