Kazi ya ujenzi wa kituo cha mkutano kinachojengwa na China yakamilika kwa asilimia 85 Zambia
2022-02-09 09:44:18| CRI

Ofisa wa serikali ya Zambia jana alisema kazi ya ujenzi wa Kituo cha mkutano cha kimataifa cha Kenneth Kaunda imekamilika kwa asilimia 85, ambacho ni kituo cha kisasa kilichoko mjini Lusaka nchini humo na mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika wa mwaka huu utafanyika kwenye jengo hilo.

Shirika la utangazaji la Zambia limemnukuu msimamizi wa majengo kwenye idara ya miundombinu ya umma Tadalisika Zulu akisema kuwa kituo hicho cha mikutano kinajengwa na Kampuni ya uchumi na teknolojia ya kimataifa ya Jiangsu, China, ambayo inajitahidi ili kuikabidhi serikali ya Zambia mradi huo mwezi Machi, muda ambao ni kabla ya mwezi uliopangwa awali wa Aprili mwaka huu. Ameongeza kuwa jengo hilo lililoanza kujengwa mwaka 2020, linaweza kubeba watu elfu nne na kazi kuu ya ujenzi huo imekamilika.