Bunge la Umma la China lakemea mswada wa sheria ya Marekani wenye maudhui hasi dhidi ya China
2022-02-09 09:46:04| CRI

Bunge la Umma la China NPC limeeleza kutoridhishwa kwake na kukemea vikali mswada wa sheria ya Marekani wenye maudhui hasi dhidi ya China.

Kwenye taarifa yake Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Umma la China, imesema Mswada huo uitwao “Sheria ya Ushindani ya Marekani ya 2022” uliopitishwa hivi karibuni na Baraza la chini la Bunge la Marekani, unachochea mawazo ya vita baridi na mtazamo wa kunufaisha upande mmoja, na kudhalilisha njia ya maendeleo ya China pamoja na sera zake za ndani na za kigeni.

Taarifa imeongeza kuwa mswada huo ulio chini ya kivuli cha kuboresha ushindani wa Marekani, unalenga kukabiliana na kukandamiza uvumbuzi na maendeleo ya China na kudumisha umwamba wa Marekani. Imesema hatua ya kuifanya China kama mshindani wa kimkakati wa Marekani itaondoa uaminfu kati ya nchi mbili, kuharibu ushirikiano wa pande mbili katika nyanja za uchumi na biashara, elimu, sayansi na tekniolojia, na hatimaye kuharibu maslahi muhimu ya Marekani.