Polisi wanachunguza vitisho vya mabomu dhidi ya shule sita karibu na Washington
2022-02-10 09:30:51| CRI

Polisi wanachunguza vitisho vya mabomu dhidi ya shule sita karibu na Washington_fororder_Washington

Polisi mjini Washington wanachunguza vitisho vya mabomu dhidi ya shule sita karibu na mji mkuu huo wa Marekani.

Watu wanahamishwa kutoka kwenye shule hizo ikiwemo shule ya sekondari ya juu ya Dunbar. Uhamisho huo ulikuja siku moja baada ya mume wa makamu wa rais wa Marekani Doug Emhoff kusindikizwa na kuondolewa kwenye shughuli moja katika shule ya Dunbar kutokana na tishio la bomu.

Vyuo vikuu zaidi ya 10 vyenye historia vya watu weusi kote nchini Marekani pia vilipata vitisho vya mabomu mapema mwezi huu, siku za kusherehekea mafanikio na mapambano ya Wamarekani wenye asili ya Afrika katika historia ya Marekani.

Imefahamika kuwa Shirika la Upelelezi la Marekani FBI limetambua watu sita ambao wote ni vijana wanashukiwa kutoa vitisho dhidi ya shule hizo za watu weusi.