Mjumbe wa China katika UM ahimiza dunia kuzingatia matishio ya kigaidi yanayotolewa na EIM/TIP
2022-02-10 09:29:18| CRI

Mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Zhang Jun ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuzingatia kwa makini matishio ya kigaidi yanayotolewa na Kundi la Harakati ya Kiislamu ya Turkistan Mashariki/Chama cha Kiislamu cha Tukistan (ETIM/TIP).

Akinukuu ripoti ya katibu mkuu, ambayo inabainisha kuwa kundi la ISIS linaendelea kuajiri wapiganaji kutoka ETIM/TIP, Zhang Jun amesema China “ina wasiwasi mkubwa” juu ya hali hii.

Zhang amesema ETIM ni kundi la kigaidi linaloorodheshwa na Kamati ya 1267 ya Baraza la Usalama, ambalo limefanya mashambulizi mengi yasiyo ya kibinadamu mkoani Xinjiang, China, na kuleta hasara kubwa kwa raia.

Balozi huyo alisema katika miaka ya hivi karibuni, kundi hilo limeenea katika Asia ya Kati na ya Kusini, Mashariki ya Kati na maeneo mengine, akiongeza kuwa ripoti iliyotolewa na kikundi cha ufuatiliaji cha Kamati ya 1267 mapema mwezi huu imeonesha kuwa, kuna wapiganaji 1,000 hadi 3,000 wa ETIM/TIP nchini Syria.