Rais wa Iran asema kutuma timu kwenda Vienna kunaonyesha dhamira yake ya kutafuta ufumbuzi wa kidiplomasia
2022-02-11 09:46:42| CRI

Rais Ebrahim Raisi wa Iran jana alisema kutuma timu mjini Vienna kwa ajili ya kushiriki mazungumzo ya juu ya suala la kurejesha makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 kunaonyesha dhamira ya dhati ya Iran ya kutafuta ufumbuzi wa kidiplomasia.

Raisi alisema hayo alipokutana na mabalozi wa nchi za kigeni nchini Iran katika maadhimisho ya miaka 43 ya Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979 ya Iran. Amesema Iran inajitahidi kushiriki kwenye mazungumzo kwa hiari siku zote. Hali ya sasa juu ya makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 yanayofahamika kama mpango wa pamoja wa pande zote wa utekelezaji makubaliano (JCPOA) inasababishwa na kushindwa kwa Marekani kutekeleza ahadi yake juu ya makubaliano hayo pamoja na kutochukua hatua kwa pande husika dhidi ya vikwazo.

Amesisitiza kuwa Iran siku zote inafuatilia umuhimu wa kuishi kwa amani, na inahitaji kujitahidi kuhimiza mambo ya kidiplomasia ya kiujenzi kwa ajili ya kutatua masuala ya kikanda na ya kimataifa.