Marekani yakwepa kuwajibika kwa shughuli za satelaiti za Starlink
2022-02-11 09:49:34| CRI

Marekani yakwepa kuwajibika kwa shughuli za satelaiti za Starlink_fororder_9

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China Zhao Lijian amesema Marekani inakwepa wajibu wake na kuhamishia ufuatiliaji wa kile kinachojulikana kama “vigezo vya  mgongano wa dharura”, ambao si msimamo wa kuwajibika wa nchi yenye uwezo mkubwa katika anga ya juu inayopaswa kuwa nao.

Msemaji Zhao alisema hayo katika mkutano na waandishi wa habari akijibu swali kwamba Marekani inakanusha kauli ya China kwamba satelaiti za Starlink zilihatarisha kituo cha anga za juu cha China mara mbili katika barua iliyotumwa kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya anga za juu Januari 28 huko Vienna.

Zhao amesema katika hatua zinazohusika za kuepusha mgongano, satelaiti za Starlink za Marekani ziko katika hali ya kuendelea kuzunguka obiti, na mikakati na nia zao za uendeshaji hazijulikani.

Zhao ameongeza kuwa baada ya matukio hayo, viongozi wa China walijaribu mara kadhaa kuwasiliana na upande wa Marekani kupitia barua pepe, lakini hawakujibiwa.