Serikali ya Ukraine yatangaza kuwa haijafunga anga yake
2022-02-14 09:07:26| CRI

Serikali ya Ukraine yatangaza kuwa haijafunga anga yake_fororder_VCG111369091365

Wizara ya miundombinu ya Ukraine imetoa taarifa ikisema Ukraine haijafunga anga yake na haijaweka vizuizi kwa mashirika ya ndege yanayoendelea na kazi nchini humo.

Taarifa hiyo imesema habari kuhusu Ukraine kufunga anga yake ni uongo, serikali ya Ukraine haijafanya uamuzi huu, na mashirika mengi ya ndege nchini Ukraine yanaendelea kufanya kazi kama kawaida.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Ukraine, kampuni ya kimataifa ya bima jana iliarifu shirika la ndege la Ukraine kwamba itasitisha huduma za bima kwa ndege zinazosafiri katika anga ya Ukraine ndani ya saa 48.

Taarifa hiyo imesema mabadiliko ya sasa katika soko la bima yamesababisha ugumu kwa baadhi ya mashirika ya ndege, na Ukraine iko tayari kuchukua hatua za kutoa uhakikisho wa kifedha kwa soko la usafiri wa anga.