UM wakamilisha kipindi cha kwanza cha mashauriano nchini Sudan kwa ajili ya kumaliza msukosuko wa kisiasa
2022-02-14 08:31:13| CRI

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan UNITAMS jana Jumapili ilikamilisha kipindi cha kwanza cha mashauriano na pande husika za nchi hiyo yanayolenga kumaliza msukosuko wa kisasa nchini humo.

UNITAMS itatoa waraka unaojumuisha maeneo makuu ya mwafaka uliofikiwa kati ya makundi ya kisiasa nchini Sudan juu ya mpito wa kuelekea utawala wa kiraia.

Mkuu wa tume hiyo Volker Perthes ameutaka mchakato huo wa mashauriano kuwa “wenye maana” kwa kuwa umeiruhusu tume yake kusikiliza maoni na mapendekezo mbalimbali kutoka kwa watu wa Sudan.