Chapa tatu za China ni kati ya kampuni tano bora za simu za kisasa duniani
2022-02-14 09:01:08| CRI

Kwa mujibu wa kampuni ya utafiti wa soko la teknolojia Canalys, chapa za simu za kisasa za China ikiwemo Xiaomi, Oppo na Vivo ni kati ya chapa tano bora za simu za kisasa duniani kutokana na mauzo katika mwaka jana.

Xiaomi imeshika nafasi ya tatu kwa mauzo kwa mwaka 2021 uliongezeka kwa asilimia 28 hadi kufikia simu milioni 191.2. Inafuatwa na Oppo ikiwa na ongezeko la asilimia 22 kwa kuuza simu milioni 145.1, huku Vivo ikishika nafasi ya tano kwa kuuza simu milioni 129.9 mwaka jana.

Samsung ilishika nafasi ya kwanza kwa kuuza simu milioni 275, huku Apple ikishika nafasi ya pili kwa kuuza simu milioni 230.

Takwimu za Canalys zimeonesha kuwa wafanyabiashara wa rejareja wa simu za mkononi waliuza jumla ya simu bilioni 1.35 za kisasa duniani mwaka jana, likiwa ni ongezeko la asilimia 7 ikilinganishwa na mwaka 2020 na kukaribia bilioni 1.37 ya mwaka 2019.