Tanzania yachukua hatua kushughulikia suala la kupanda kwa bei ya mbolea
2022-02-15 09:11:26| CRI

Mamlaka nchini Tanzania imesema inachukua hatua zenye lengo la kushughulikia tatizo la kupanda kwa bei ya mbolea lililotokana na changamoto za COVID-19.

Waziri wa Kilimo wa Tanzania Bw. Hussein Bashe amesema serikali imepanga hatua za muda mfupi na mrefu, ambazo ni pamoja na kuhakikisha kuwa bandari zinatoa kipaumbele kwenye kushusha mbolea bandarini na kupunguza tozo za mbolea, kusafirisha mbolea kwa njia ya reli, na kuhimiza matumizi ya mbolea mbadala na kuruhusu ushindani kwenye uagizaji wa mbolea.

Hatua za muda mrefu ni pamoja na kuhimiza ujenzi wa viwanda vya mbolea.