Madagaska kukabiliwa na kimbunga kingine
2022-02-15 09:33:51| CRI

Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema kuwa Madagaska itakabiliwa na kimbunga kingine siku 10 tu baada ya watu 121 kufa katika kimbunga cha Batsirai.

Kimbunga Batsirai kiliikumba sehemu ya kusini-mashariki mwa Madagaska tarehe 5 mwezi Februari, na kusababisha kuharibika kwa makazi ya watu 29,000 na karibu nyumba 19,000.

Msemaji huyo amesema shirika la mpango wa chakula Duniani WFP litatoa fedha bila masharti kuzisaidia familia zilizoathiriwa kwa muda wa miezi mitatu ijayo. Shirika la afya Duniani pia limeunga mkono kurudisha huduma za afya na kukarabati miundombinu ya matibabu iliyoharibiwa na kimbunga.