Bach atoa Tuzo ya Heshima ya IOC kwa mkuu wa CMG
2022-02-15 21:04:11| Cri

Rais wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa IOC Thomas Bach amelipongeza Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG kwa kuitangaza kwa mafanikio Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya mwaka 2022.

Alipokutana na mkuu wa CMG Shen Haixiong, Bach amepongeza sana idadi kubwa ya watazamaji wa michezo hiyo ambayo haijawahi kupatikana katika historia ya michezo hiyo. Hadi kufikia Februari 10, idadi ya watazamaji wa michezo hiyo kupitia jukwaa la CMG imezidi milioni 500.

Bach pia ametoa Tuzo ya Heshima ya Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa kwa mkuu wa CMG Shen Haixiong, kutokana na mafanikio iliyoyapata CMG na ushirikiano wa kiwenzi na ushirikiano kati ya CMG na IOC.