Raia wa Afghanistan wafanya maandamano ya kupinga Marekani kunyakua raslimali za nchi yao
2022-02-16 09:28:43| cri

Maelfu ya raia wa Afghanistan waliandamana tarehe 15 mwezi huu kupinga Marekani kunyakua raslimali za nchi yao na kulaani kitendo hicho kuwa ni wizi wa wazi. Mwandaaji mmoja wa maandamano hayo amesema maandamano yamefanyika katika miji mikuwa yote nchini humo.

Tangazo lililotolewa na waandamanaji limesema kitendo cha Marekani kimekiuka sheria ya kimataifa na kutaka rais Joe Biden wa Marekani kufuta amri ya tarehe 11 inayopanga kufidia wahanga wa shambulizi la 9/11 kwa nusu ya mali za Benki kuu ya Afghanistan zilizozuiwa nchini Marekani. Tangazo linasema maandamano yataendelea hadi Marekani itakaporudisha mali za Afghanistan.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Russia Bi. Maria Zakharova amesema uamuzi huo wa Marekani si kitendo cha busara  na kimezidisha majanga ya kibinadamu nchini Afghanistan.