Kenya yazindua vifaa vya upimaji wa haraka wa COVID-19 na Malaria
2022-02-16 09:06:34| CRI

Wizara ya afya ya Kenya imezindua vifaa vya upimaji wa haraka wa Malaria na COVID-19 ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha utambuaji wa haraka na matibabu ya magonjwa hayo.

Katibu mkuu tawala wa wizara ya kilimo ya Kenya Bw. Rashid Aman, amesema vifaa hivyo vimetengenezwa na watafiti wenyeji, na vitaisaida Kenya kuagiza vifaa hivyo kutoka nje ya nchi kwa gharama kubwa.

Amesema tayari vifaa hivyo vimetengenezwa na Taasisi ya utafiti wa kimatibabu ya Kenya (KEMRI) na vimeanza kuuzwa kwenye maduka ya dawa ya Kenya. Ameongeza kuwa serikali ya Kenya itaendelea kuiunga mkono taasisi hiyo iendelee kuzalisha vifaa hivyo, na kuvinunua ili  iendelee kufanya utafiti na kuviboresha.