UM na wenzake watafuta dola milioni 190 kwa ajili ya watu wenye hali duni mashariki mwa Ukraine
2022-02-16 10:01:00| CRI

Kutokana na dunia kufuatilia hali ya Ukraine, Umoja wa Mataifa na wenzake wanatafuta dola milioni 190 za kimarekani kusaidia watu wenye hali duni zaidi mashariki mwa nchi hiyo.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia uratibu wa mambo ya kibinadamu OCHA imesema, inafuatilia mahitaji na ulinzi wa watu milioni 2.9 walioko katika “mstari wa mawasiliano” kati ya Donetsk na Luhansk, wakati jumuiya ya kimataifa ikifuatilia katika hali ya wasiwasi katika mpaka kati ya Ukraine na Russia.

Ofisi hiyo imesema, inalenga kupunguza machungu ya watu milioni 1.8 wenye hali duni zaidi katika pande zote mbili za mstari wa mawasiliano kwa kutoa dola milioni 190 za kimarekani zinazotafutwa na ofisi hiyo katika mpango wa kibinadamu wa mwaka 2022.