Rais Xi Jinping wa China azitaka pande husika zitatue suala la Ukraine kwa njia ya kisiasa
2022-02-17 14:39:40| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kuwa pande husika zinapaswa kushikilia njia ya kisiasa kwenye utatuzi wa suala la Ukraine.

Rais Xi Jinping amesema hayo alipofanya mazungumzo na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kwa njia ya simu. Pia amesisitiza kuwa pande husika zinapaswa kutumia majukwaa mbalimbali ikiwemo Utaratibu wa Normandy, kutatua suala la Ukraine kwa njia ya mazungumzo.