Ni furaha iliyoje kuwa nawe tena msikilizaji katika kipindi hiki cha Daraja kinachokujia kila jumapili muda kama huu kupitia CMG Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing.
Katika kipindi cha leo tutakuwa na ripoti inayozungumzia China kuongeza uwekezaji katika miradi yenye utoaji mdogo wa kaboni barani Afrika ili kulisaidia bara hilo kupunguza utoaji wa hewa chafu na hivyo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Pia tutakuwa na ripoti kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili, Nairobi, kuhusu matarajio ya Kenya kushiriki mashindano yajayo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi.