Marais wa China na Ufaransa wakubaliana kuimarisha ushirikiano wa nchi zao
2022-02-17 08:40:50| CRI

Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron wamekubaliana kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zao, na pia kuimarisha uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya.

Kwenye mazungumzo yao yaliyofanyika kwa njia ya simu, Rais Macron ametoa salamu za mwaka mpya wa jadi na kuipongeza China kwa kuendesha vizuri michezo ya olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing, ambayo amesema ni kazi ngumu kwa China kuandaa michezo hiyo katika majira ya sasa, na Ufaransa inaunga mkono michezo hii.

Rais Xi pia ametoa salamu za mwaka mpya kwa Rais Macron na watu wa Ufaransa, na kupongeza mafanikio ya wanamichezo wa Ufaransa. Rais Xi pia amekumbusha mawasiliano ya mara mbili kwa njia ya simu na Rais Macron ambayo yamezaa matunda, na kufanya biashara kati ya pande hizo mbili kufikia dola za kimarekani bilioni 80.