Tanzania kuimarisha uvunaji wa maji ya mvua wakati inakabiliwa na msukosuko wa maji
2022-02-17 08:40:13| CRI

Mamlaka nchini Tanzania zimesema zinafanyia kazi mikakati yenye lengo la kuimarisha uvunaji wa maji ya mvua wakati nchi hiyo ikikumbwa na uhaba wa maji katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo.

Naibu waziri wa Maji Bibi Mary Prisca Mahundi ameliambia bunge mjini Dodoma kuwa serikali imeamua kuwekeza kwenye uvunaji wa maji badala ya kuchimba visima ambavyo havitoi maji ya kutosha.

Amesema ujenzi na ukarabati wa mabwawa ya kuhifadhia maji unaendelea katika wilaya 20. Maeneo 58 yanayofaa kwa ujenzi wa mabwawa madogo yametambuliwa, na ujenzi utafanyika katika mwaka wa fedha 2022/2023.