Sekta ya pensheni ya Kenya yatarajia ushirikiano na kampuni za China ili kuongeza mapato ya uwekezaji
2022-02-18 09:15:44| CRI

Sekta ya pensheni ya Kenya inapanga kushirikiana na kampuni za China ili kuongeza mapato yanayotokana na uwekezaji.

Mwenyekiti wa Mfuko wa Uwekezaji wa Pensheni Kenya (KEPFIC) Bw. Sundeep Raichura, amesema mjini Nairobi kuwa wanatafuta kushirikiana na mashirika ya kigeni, yakiwemo mashirika ya China, ambayo yana utaalamu wa kutekeleza miradi ya miundombinu muhimu ikiwemo barabara, reli na vituo vya kuzalisha umeme, ili kuongeza mapato yanayotokana na uwekezaji.