Dola bilioni 1.88 zahitajika kutoa misaada ya kibinadamu nchini DRC
2022-02-18 09:15:05| CRI

Mashirika ya kibinadamu yanahitaji dola bilioni 1.88 za kimarekani kutoa misaada kwa watu milioni 8.8 walio hatarini zaidi kati ya watu milioni 27 wanaokabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema serikali na mashirika ya kibinadamu wamezindua mpango wa misaada ya kibinadamu kwa mwaka 2022 unaohitaji dola bilioni 1.88 za kimarekani.

Bw. Dujarric amesema, hali ya kibinadamu nchini DRC inaendelea kuzorota, hasa kwenye mikoa ya mashariki, na mashambulizi dhidi ya raia, na mwaka jana wakiwemo wakimbizi wa ndani yameongezeka, hasa kwenye mikoa ya Ituri na Kivu kaskazini.