Wanamitindo mashuhuri waliotikisa majukwaa ya Fashion
2022-02-18 08:20:16| Cri

Neno ‘supermodel’ au wanamitindo kwa Kiswahili lilianza kutumika zamani sana tangu mwaka 1891, katika mahojiano na msanii Henry Stacy Marks kwa ajili ya Jarida la Strand, ambapo Marks alimwambia mwandishi wa habari Harry How, "Mamodo wengi ni waraibu pombe, na baada ya kukaa kwa muda, ghafla wanakwenda kulala. Kisha kuna jina ninaloliita ‘masupermodel’. Yaani aina ya mtu anaingia kwa ajili ya maonyesho. Tarehe 6 Oktoba 1942, mwandishi aitwaye Judith Cass naye alilitumia neno hili la super model kwenye makala yake katika Chicago Tribune, ambayo ilikuwa na kichwa "Super Models Are Signed for Fashion Show". Baadaye mwaka 1943, wakala anayeitwa Clyde Matthew Dessner alitumia neno hilo katika kitabu cha “namna ya kufanya” kuhusu uanamitindo, kilichoitwa So You Want to Be a Model! Mnamo 1947, mwanaanthropolojia Harold Sterling Gladwin aliandika "mwanamitindo mkuu" katika kitabu chake Men Out of Asia. Mnamo mwaka 1949, jarida la Cosmopolitan lilimtaja Anita Colby, mwanamitindo aliyelipwa zaidi wakati huo, kama "mwanamitindo bora". Kwa hiyo fani ya uanamitindo haikuanza hivi karibuni ina historia ndefu. Na katika kipindi chote hicho waliibuka wanamitindo mbalimbali waliojibebea umaarufu ambao ameshuhudia mabadiliko makubwa katika fani hii. Lakini ilikuja kushamiri zaidi katika miaka ya tisini ambayo ilikuwa ni enzi za kina Campbell, Crawford, Evangelista, Patitz and Turlington ambao hadi sasa wanachukuliwa kama Wanamitindo waanzilishi.

Hivyo katika kipindi cha leo tutaangazia wanamitindo mbalimbali wa China na Afrika ambao wamejibebea umaarufu mkubwa pamoja na kutangaza nchi zao.