Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania yatoa tahadhari kuhusu msimu wa mvua
2022-02-18 09:04:32| CRI

Mamlaka ya hali ya hewa ya Tanzania TMA imetoa tahadhari kuhusu msimu wa mvua wa mwezi Machi hadi Mei, na kusema mvua katika msimu huo zitakuwa na matokeo chanya na matokeo hasi.

Taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo imesema katika baadhi ya maeneo ya nchi kutakuwa na madhara kwenye sekta nyeti kama vile kilimo na usalama wa chakula, mifugo na uvuvi, wanyamapori na utalii, afya, maji, usafiri na nishati.

Taarifa inasema vipindi vyenye mvua kubwa vitakuwa mwezi Machi na vitayakumba maeneo ya pwani ya mashariki na mwezi Aprili eneo la nyanda za juu kaskazini mashariki.

TMA imeshauri wakulima kuandaa mashamba na kupanda mapema na kutumia mbinu zinazofaa kudhibiti mmomonyoko wa ardhi na kuondoka kwa rutuba, na kuchagua mbegu na mazao kuendana na msimu.