Shannon Abeda—Mchezaji wa Afrika Ang'arisha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi
2022-02-20 15:43:15| cri

Shannon Abeda—Mchezaji wa Afrika Ang’arisha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi_fororder_微信图片_20220220154239

Shannon Abeda mwenye umri wa miaka 25 ni mchezaji wa Eritrea aliyeshiriki kwenye shindano la kuteleza theluji mlimani (yaani Alpine Skiing Giant Slalom) katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing. Naye pia ni mmojawapo kati ya wachezaji 6 wa bara la Afrika kwenye michezo hiyo inayofanyika Februari 4 hadi 20 nchini China. Amemaliza mashindano yake kwa nafasi ya 39 ambayo haina nafasi ya kutwaa medali, lakini ameinua nafasi yake zaidi ya 20 kuliko nafasi ile katika Michezo ya Olimpiki miaka minne iliyopita.

Shannon Abeda alionekana katika jukwaa la Olimpiki kwa mara ya kwanza mwaka 2018 huko Pyeongchang. Baadaye aliwahi kustaafu kwa sababu ya majeraha na magonjwa yake. Lakini kifo cha ghafla cha rafiki yake kilimfanya kijana huyo aangalie maisha yake na masikitiko ya maishani tena. Mnamo Novemba 2020, Shannon Abeba alirudi katika mchezo huo akiwa anatamani Waafrika wengi zaidi washiriki kwenye michezo ya majira ya baridi kupitia Michezo ya Olimpiki ya Beijing.

(Habari hii inatokana na tovuti rasmi ya Kamati ya maandalizi ya Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Paralimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing.)