Mwenyekiti wa IOC Thomas Bach apongeza CMG kwa kazi nzuri ya utangazaji wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing
2022-02-20 19:34:20| cri

Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) Thomas Bach amelipongeza Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) kwa kazi yake hodari ya utangazaji wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing wakati alipomwandikia mkuu wa CMG Shen Haixiong tarehe 19 mwezi huu ambapo michezo hiyo inakaribia kumalizika.

Bach alisisitiza kwamba idadi kubwa ya watazamaji wa michezo hiyo inaonyesha kuongezeka kwa hamu ya watu wa China juu ya michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi. Alishukuru juhudi za CMG katika kuhimiza michezo ya Olimpiki na moyo wa Olimpiki kwa niaba ya kamati yake. Alisema Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki intarajia ushirikiano na CMG katika siku za mbele kwa kupanua ushawishi wa Michezo ya Olimpiki na kuhimiza michezo kukita mizizi kati ya watu wa China.
Bach alipozungumiza na mwandishi wa habari wa CMG tarehe 20 mwezi huu alisema, sasa kumekuwa na wachina milioni 300 ambao wameshiriki kwenye michezo ya majira ya baridi, hali inayoonesha mustakbali mkubwa wa michezo hiyo nchini China. Inakadiriwa kuwa thamani ya soko la michezo ya majira ya baridi nchini China itakuwa dola za kimarekani bilioni 150 ifikapo mwaka 2025, kiasi ambacho kitatoa msukumo mkubwa katika kuhimiza michezo ya majira ya baridi duniani.