Nafasi ya miundombinu barani Afrika baada ya janga la COVID-19 kupewa kipaumbele katika Wiki ya PIDA
2022-02-21 08:35:52| CRI

Wataalamu na watunga sera barani Afrika wanatarajiwa kujadili nafasi ya sekta ya miundombinu katika kuchochea ufufukaji baada ya janga la COVID-19, ukuaji na unyumbukaji katika Afrika kwenye Program ya 7 ya Wiki ya Maendeleo ya Miundombinu barani Afrika (PIDA) inayotarajiwa kuanza wiki ijayo.

Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Afrika imesema, Wiki hiyo itakayoanza Februari 28 hadi Machi 4 jijini Nairobi, Kenya, itafanyika kwa njia ya mtandao na moja kwa moja, na itajadili kwa jinsi gani Afrika itaongoza katika maendeleo ya miundombinu baada ya janga la COVID-19 pamoja na kuunga mkono masuala muhimu ya kiuchumi na kijamii katika bara hilo kwenye zama za kidijitali.

Taarifa hiyo pia imesema, mwaka huu, Wiki hiyo inaadhimishwa wakati kuna wasiwasi mkubwa unaoendelea wa kiuchumi na kijamii duniani kutokana na janga la COVID-19, ambalo limeleta athari kubwa za kiuchumi na kijamii zilizoathiri viashiria vya maendeleo ya binadamu barani Afrika.