Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing yafungwa
2022-02-21 08:36:28| CRI

Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing imemalizika jana baada ya siku 16 za michezo mbalimbali ya wanariadha na matukio mazuri yaliyoashiria umoja na urafiki.

Rais Xi Jinping wa China alihudhuria sherehe za kufungwa kwa Michezo hiyo katika Uwanja wa michezo wa Kiota cha Ndege, ambapo kabla ya kutangaza kufungwa, rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Thomas Batch aliielezea michezo hiyo kuwa ya kipekee. Amesema moyo wa Olimpiki uliweza kung’ara zaidi kwa sababu Wachina waliweka jukwaa kwa njia ambayo ni bora zaidi na salama zaidi.

Mji wa Beijing kwa sasa umekuwa mji pekee wa kwanza kuandaa Michzo ya Olimpiki ya Majira ya Joto na Baridi.