Uuzaji wa bidhaa za photovoltaic za China nje ya nchi wapanda kwa asilimia 60 mwaka 2021
2022-02-21 16:04:16| CRI

China imeshuhudia uuzaji mwingi wa bidhaa zake za photovoltaic (PV) nje ya nchi mwaka jana wakati dunia inaongeza juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.  Kwa mujibu wa Wizara ya Viwanda na TEHAMA, mwaka 2021 uuzaji nje wa bidhaa za PV za China ulipita dola za kimarekani bilioni 28.4, ikilinganishwa na bilioni 18.23 za mwaka uliotangulia.

China, ikiwa ni mzalishaji mkubwa zaidi wa bidhaa za nishati ya jua duniani, iliongeza uwezo wa kuzalisha gigawati 53 za umeme kwa nishati ya juu mwaka 2021. China sasa imeweka peneli nyingi za nishati ya jua kwenye mapaa ya majengo kote nchini, ambayo yanaweza kuzalisha gigawati 108 za umeme, kiasi ambacho ni kikubwa zaidi kuliko sehemu yoyote nyingine duniani.

Ili kutimiza lengo lake la kufikia uwiano kati ya utoaji na ufyonzaji wa hewa ya ukaa (Carbon Neutrality) ifikapo mwaka 2060, China inalenga kuwa na nishati endelevu, ikiwemo nishati ya jua na ya upepo, inayoweza kuchangia asilimia 80 ya vyanzo vyake vya nishati ifikapo mwaka 2060.