Malkia Elizabeth II wa Uingereza akutwa na maambukizi ya COVID-19
2022-02-21 08:37:32| CRI

Kasri ya Buckingham jana imethibitisha kuwa, Malkia Elizabeth II wa Uingereza amekutwa na mambukizi ya COVID-19.

Kasri hiyo inasema, Malkia ana dalili ndogo ya mafua, lakini anatarajiwa kuendelea na kazi rahisi katika makazi yake yaliyoko Windsor.

Taarifa hiyo imekuja wiki chache baada ya Malkia Elizabeth II kuadhimisha miaka 70 tangu ashike madaraka, na imefahamika kuwa amepata dozi tatu za chanjo ya COVID-19.