Iran yasema bado kuna masuala muhimu yanayohitaji kutatuliwa katika mazungumzo ya nyuklia
2022-02-22 09:06:45| CRI

Iran yasema bado kuna masuala muhimu yanayohitaji kutatuliwa katika mazungumzo ya nyuklia_fororder_伊朗外交部发言人Saeed Khatibzadeh

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Saeed Khatibzadeh amesema, mazungumzo kati ya pande zinazohusika kuhusu makubaliano ya suala la nyuklia la Iran yanayofanyika huko Vienna yamepiga hatua kubwa, lakini bado kuna masuala muhimu yanayohitaji kutatuliwa.

Khatibzadeh amesema ujumbe wa Iran umetoa mapendekezo kwa pande zinazohusika katika mazungumzo hayo ili kutatua masuala yaliyosalia, na Iran inasubiri uamuzi kutoka nchi za Ulaya na Marekani, lakini bado haijaona nia yao.

Khatibzadeh amesema Iran kamwe haitarudi nyuma katika masuala yanayohusu haki za watu wake, haswa vikwazo vyote vinavyozuia manufaa ya kiuchumi ya Iran lazima viondolewe.