Rais wa Russia asaini tangazo linalotambua nchi mbili huru mashariki mwa Ukraine
2022-02-22 08:43:47| CRI

Rais wa Russia Vladmir Putin amesaini matangazo mawili yanayotambua “Jamhuri ya Watu wa Lugansk (LPR)” na “Jamhuri ya Watu wa Donetsk (DPR)” kama nchi mbili huru na zenye mamlaka.

Katika hafla iliyofanyika ikulu ya Russia, rais Putin pia alisaini Mkataba wa Urafiki, Ushirikiano na Kusaidiana kati ya Rusia na wakuu wa nchi hizo mbili. Baada ya kuzitambua nchi hizo mbili, rais Putin ametoa maelekezo kwa jeshi la ulinzi la Russia kuhakikisha usalama katika nchi hizo.