China yatoa mpango wa miaka mitano wa huduma za wazee
2022-02-22 08:43:17| CRI

China yatoa mpango wa miaka mitano wa huduma za wazee_fororder_VCG11493528679

Baraza la Serikali la China limetoa mpango wa maendeleo ya mfumo wa huduma za wazee nchini humo katika kipindi cha Mpango wa 14 wa Miaka Mitano (2021-2025), katika hatua mpya ya kutekeleza mkakati wa kitaifa kukabiliana na wazee.

Mpango huo unaweka wazi malengo makuu na majukumu ya kipindi hicho cha miaka mitano, ikiwemo kuongeza upatikanaji wa huduma kwa wazee, kuboresha muundo ili kusaidia afya ya wazee, na kuendeleza uvumbuzi na maingiliano ya mifumo ya huduma.

Majukumu yaliyofafanuliwa ni pamoja na kuimarisha usalama wa huduma kwa wazee, kupanua maeneo jumuishi ya huduma, na kulinda maslahi halali ya wazee.