Watu 59 wafariki katika mlipuko wa mgodi wa dhahabu kusini magharibi mwa Burkina Faso
2022-02-22 09:16:27| cri

Watu 59 wafariki katika mlipuko wa mgodi wa dhahabu kusini magharibi mwa Burkina Faso_fororder_webwxgetmsgimg (2)

Watu 59 wamefariki na wengine 55 kujeruhiwa katika mlipuko wa mgodi wa dhahabu uliotokea jana huko Gbomblora, mkoa wa Poni, kusini magharibi mwa Burkina Faso.

Chanzo cha mlipuko huo bado hakijajulikana, lakini mashuhuda kadhaa walieleza kuwa mlipuko huo ulitokana na moto ambao uliteketeza vilipuzi vinavyotumiwa na wachimbaji dhahabu wakati wa shughuli zao.