Mali yapitisha mkataba mpya kuongeza muda wa mpito wa kisiasa
2022-02-23 08:23:14| cri

Baraza la Kitaifa la Mpito la Mali limepitisha mkataba mpya unaoongeza muda wa mpito wa kisiasa nchini humo.

Kwa mujibu wa mkataba huo mpya, kipindi cha mpito wa kisiasa kitaongezwa kutoka miezi 6 hadi miaka 5, pia mkataba huo umemzuia rais wa mpito wa nchi hiyo kushiriki katika uchaguzi ujao wa rais na kuondoa nafasi ya makamu wa rais.

Taarifa iliyotolewa na Kamati ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imesema, itapeleka ujumbe utakaoongozwa na Rais wa zamani wa Nigeria Bw. Goodluck Jonathan nchini Mali kujadili mchakato ujao wa kisiasa wa nchi hiyo.