Bw. Xue Bing ateuliwa kuwa mwakilishi maalumu wa China kwenye kanda ya Pembe ya Afrika
2022-02-23 10:52:24| cri

Bw. Xue Bing ateuliwa kuwa mwakilishi maalumu wa China kwenye kanda ya Pembe ya Afrika_fororder_src=http___bkimg.cdn.bcebos.com_pic_e61190ef76c6a7efaa35be91f8faaf51f3de6671&refer=http___bkimg.cdn.bcebos

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema, China imemteua Bw. Xue Bing kuwa mwakilishi maalumu wa wizara hiyo kwenye kanda ya Pembe ya Afrika.

Bw. Xue aliwahi kuwa balozi wa China nchini Papua New Guinea, na kufanya kazi katika nchi tofauti za Afrika, Amerika na Oceania.

Bw. Wang amesema ikiwa rafiki wa nchi za Pembe ya Afrika, China siku zote inafanya juhudi kwa ajili ya amani, utulivu na maendeleo ya kanda hiyo. Pia amesema Bw. Xue atajenga uhusiano wa kikazi pamoja na wenzake wa pande mbalimbali mapema, na kuwasiliana nao kwa karibu kuhuku kuhimiza utekelezaji wa Mpango wa maendeleo ya amani ya Pembe ya Afrika uliotolewa na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi alipofanya ziara barani Afrika mwanzoni mwa mwaka huu.