Rais wa Ukraine asema anafikiria kusitisha uhusiano wa kibalozi na Russia
2022-02-23 09:18:07| CRI

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine ameilaani Russia kushambulia mamlaka na ukamilifu wa ardhi ya nchi yake, pia kwa kutambua uhuru wa Donetsk na Luhansk zilizo mashariki mwa Ukraine, na kusema anafikiria kusitisha uhusiano wa kibalozi na Russia.

Rais Zelensky amesema kitendo cha Russia kinamaanisha kuwa nchi hiyo imejitoa kwenye Mikataba ya Minsk kwa upande mmoja, na kupuuza uamuzi wa pande nne wa Mfumo wa Normandy. Amependekeza kuitisha mkutano wa dharura wa Mfumo huo, na kuahidi kuwa Ukraine itajitahidi kutatua migogoro kwa njia ya kisiasa na kidiplomasia, lakini haitavumilia uchokozi.