Waziri wa mambo ya nje wa China atoa pongezi za maadhimisho ya miaka 38 ya uhuru kwa waziri wa mambo ya nje wa Brunei
2022-02-23 16:50:28| CRI

Waziri wa mambo ya nje Bw. Wang Yi ametoa pongezi kwa njia ya simu kwa waziri wa mambo ya nje wa Brunei Bw. Dato Erywan Pehin Yusof kwa nchi hiyo kuadhimisha miaka 38 tangu nchi hiyo ijipatie uhuru.

Bw. Wang amesema mwaka jana Brunei ilikuwa nchi mwenyekiti wa zamu wa Jumuiya ya nchi za Asia Mashariki Kusini ASEAN, na uhusiano kati ya China na Jumuiya hiyo umeinuliwa kwa hatua madhubuti, wakati pande mbili zikiadhimisha miaka 30 tangu zianzishe mfumo wa mazungumzo. Mwaka jana pia ulikuwa maadhimisho ya miaka 30 tangu China na Brunei zianzishe uhusiano wa kibalozi, nchi hizo mbili zimefikia makubaliano kuhusu uhusiano huo na masuala ya kikanda na kimataifa yanayofuatiliwa na pande mbili.