Rais wa China aipongeza Brunei kuadhimisha ya miaka 38 ya uhuru
2022-02-23 16:51:26| CRI

Rais Xi Jinping wa China leo ametoa ujumbe wa pongezi kwa Sultani Haji Hassanal Bolkiah wa Brunei akipongeza maadhimisho ya miaka 38 tangu nchi hiyo ijipatie uhuru.

Rais Xi amesema katika miaka 38 iliyopita tangu Brunei ijipatie uhuru, chini ya uongozi wa Sultani, ujenzi wa taifa wa nchi hiyo umepata maendeleo makubwa, na kiwango cha maisha ya watu kimeinuka siku hadi siku. Mwaka jana Brunei ilikuwa mwenyekiti wa zamu wa Jumuiya ya nchi za Asia Mashariki Kusini ASEAN, na kuongoza pamoja na China mkutano wa kilele wa makumbusho ya miaka 30 tangu China na Jumuiya ya ASEAN kuanzisha mfumo wa mazungumzo na kuinua uhusiano kati ya pande mbili katika kiwango cha juu zaidi.

Rais Xi amesisitiza kuwa China na Brunei ni nchi jirani na marafiki wa jadi, na wenzi wa ushirikiano wa kimkakati, huku pande mbili zikipata mafanikio mengi ya ushirikiano katika sekta mbalimbali. Rais Xi amesema anatilia maanani maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.