Maspika wa Bunge la China na Algeria wafanya mazungumza
2022-02-23 08:07:33| CRI

Spika wa Bunge la Umma la China Bw. Li Zhanshu jana amefanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Algeria Ibrahim Boughali kwa njia ya video.

Bw. Li Zhanshu amesisitiza kuwa, mawasiliano kati ya mabunge ya nchi hizo mbili ni sehemu muhimu ya ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Algeria. Amesema Bunge la China na Bunge la Algeria zinapenda kuimarisha mawasiliano katika ngazi mbalimbali, na kubadilishana uzoefu wa kutunga sheria na usimamizi katika mambo kadhaa ikiwemo mambo ya fedha, kilimo, elimu, na uwekezaji wa nchi za nje. Pia kuongeza utaratibu katika shughuli za pande nyingi, ili kutoa mchango kwa ajili ya maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Bw. Boughali amesema Algeria inatumai kupanua zaidi ushirikiano kati yake na China katika sekta mbalimbali ikiwemo uchumi na biashara, uwekezaji, sayansi na teknolojia, utamaduni, na mapambano dhidi ya COVID-19.