Rais wa China apongeza uzinduzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere
2022-02-24 08:56:25| CRI

Rais wa China apongeza uzinduzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere_fororder_timg (39)

Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za pongezi kwa uzinduzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere iliyofanyika Kibaha, mkoa wa Pwani, nchini Tanzania.

Chuo hicho kimejengwa kwa pamoja na Chama cha Mapinduzi cha Tanzania, Chama cha African National Congress cha Afrika Kusini, Chama cha Ukombozi cha Msumbiji, Chama cha Harakati ya Ukombozi wa Watu cha Angola, Chama cha SWAPO cha Namibia, na Chama cha ZANU-PF cha Zimbabwe

Rais Xi ametoa salamu hizo kwa niaba yake na kwa niaba ya Chama cha Kikomunisti cha China. Amesema kwa muda mrefu, vyama hivyo 6 vimeongoza wananchi wao kujipatia uhuru na kuendeleza nchi zao, na Chuo hicho kitatoa jukwaa muhimu kwa vyama hivyo kujikamilisha na kuongeza uwezo wa utawala, ili kutimiza ustawi wa nchi zao na kuleta manufaa kwa wananchi wao.

Rais Xi amesisitiza kuwa, hivi sasa dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayajatokea katika miaka 100 iliyopita, na China na Afrika zinahitaji kuimarisha mshikamano na ushirikiano, ili kukabiliana na changamoto na kuhimiza maendeleo.