Ukraine yatangaza sheria ya kijeshi kufuatia operesheni ya kijeshi ya Russia
2022-02-24 15:02:58| Cri

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky leo ametangaza sheria ya kijeshi nchini humo, baada ya Russia kuanza operesheni yake ya kijeshi dhidi ya Ukraine.

Akihutubia kwa njia ya video, Zelensky amesema nchi yake inashambuliwa. Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, maghala na viwanja vya ndege vya kijeshi katika mji mkuu vilishambuliwa kwa makombora.

Ripoti za vyombo vya habari zinasema mjini Kiev, milipuko ilisikika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Boryspil na maeneo mengine ya mji, ambapo anga ya nchi hiyo imefungwa kwa ndege za kiraia.