Rais wa China awataka wanariadha wa michezo ya majira ya baridi wa China kufanya juhudi zaidi kwa ajili ya taifa na watu
2022-02-25 08:47:11| cri

Rais Xi Jinping wa China jana aliwataka wanariadha wa michezo ya majira ya baridi wa China kujitahidi kuwa na "maisha mazuri" na kujitolea ujana na nguvu zao kwa taifa lao na watu wake.

Rais Xi amesema hayo alipojibu barua ya mwanariadha wa China Bw. Su Yiming. Katika barua hiyo, rais Xi alitoa pongezi kwa Su na wanariadha wengine wa michezo ya majira ya baridi kwa kufanya vizuri katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing.

Rais Xi amesema, matumaini yake kwa vijana wa China ni kuweka nchi moyoni, kuwa na malenga ya juu na kutosahau nchi yao.