China yaunga mkono mazungumzo yafanyike kati ya Russia na Ukraine
2022-02-26 00:32:24| cri

Uchambuzi: China yaunga mkono mazungumzo yafanyike kati ya Russia na Ukraine_fororder_mmexport7f3e39aba0e9d4e3e7fe6f5f0405bbfe_1645806512238

Rais Xi Jinping wa China tarehe 25 alipoongea na rais Vladimir Putin wa Russia kwa njia ya simu, alisema China inajiamulia msimamo wake kwa mujibu wa uchunguzi wa hali halisi ya suala la Ukraine. Alisisitiza umuhimu wa kuachilia mbali mawazo ya vita baridi, kuzingatia na kuheshimu matakwa ya haki ya nchi mbalimbali katika masuala yanayohusu usalama wan chi hizo, na kufikisha mfumo endelevu wenye uwiano na ufanisi wa usalama barani Ulaya kwa njia ya mazungumzo. Rais Xi amesema kuwa, China inaunga mkono mazungumzo yafanyike kati ya Russia na Ukraine ili kutafuta ufumbuzi wa masuala. Rais Putin alieleza nia ya kufanya mazungumzo ya ngazi ya juu na Ukraine.

Hayo ni maongezi muhimu, pia ni jitihada mpya zilizofanywa na China kwa kuchangia ufumbuzi wa kisiasa wa suala la Ukraine. Kwenye mazungumzo hayo kati ya marais wa China na Russia, pia tumesoma habari muhimu kwamba, mbali na kulipuka kwa mapigano ya kijeshi, fursa ya kufanya mazungumzo kati ya Russia na Ukraine bado ipo. Tarehe 24 Russia ilisema, endapo Ukraine iko tayari kufanya mazungumzo kuhusu nchi hiyo kutopendelea upande wowote na kutofunga silaha nchini humo, Russia inapenda kufanya mazungumzo na Ukraine. Rais Putin alipoongea na rais Xi tarehe 25, alisisitiza nia hiyo hiyo ya Russia. Na mapema ya tarehe 25, rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine alisema, “Hatuogopi kufanya mazungumzo na Russia, tuko tayari kujadiliana nao masuala yote.”

Watu wameona, wakati wa kueleza nia ya kufanya mazungumzo na Russia, rais Zelensky pia alieleza kusikitika na Jumuiya ya NATO. Alisema alishawauliza viongozi wa nchi 27 za Ulaya kuhusu kama Ukraine inaweza kujiunga na NATO, lakini hakupata jibu lolote. Rais huyo alisema “Ukraine imeachiliwa mbali na nchi za Magharibi.”

Jumuiya ya NATO inayoongozwa na Marekani inapaswa kuwajibika kwa jinsi suala la Ukraine linavyofikia hali ilivyo sasa. Baada ya kumalizika kwa vita baridi, chini ya juhudi za Marekani, NATO ilipanua wigo lake kwa mara tano kuelekea Mashariki, ikiendelea kuathiri usalama wa kimazingira katika eneo la karibu na Russia, hali ambayo kimsingi inasababisha hali ya wasiwasi kati ya Russia na Marekani na NATO. Toka mwaka 2014, Marekani iliipelekea Ukraine misaada ya kijeshi yenye thamani ya dola zaidi ya bilioni 1 za kimarekani, na mazoezi makubwa ya kijeshi yaliyofanywa mara kwa mara na NATO na Ukraine yaliisukuma Ukraine ifikie mstari wa mbele wa kuikabili Russia. Hayo yote yaliipatia Ukraine taswira kwamba, inaweza kulindwa na Marekani na NATO. Lakini wakati Ukraine ilipotoa ombi la kujiunga na NATO, ilikataliwa. Ukweli ni kwamba, Ukraine ni kifaa tu cha kuikabili Russia, lakini Nato inayoongozwa na Marekani kamwe haikubali kujitumbukizwa matatizoni.

Dalili za Marekani kuiachilia mbali Ukraine zilikuwa zimeonyeshwa hivi karibuni, kwamba ingawa ilikuwa inaendelea kuipelekea Ukraine silaha, Marekani inasisitiza mara kadhaa kuwa haitapelekea Ukraine wanajeshi kushiriki vita. Ni kama mbunge wa zamani wa Marekani Bi Tulsi Gabbard alivyosema hivi majuzi kuwa, serikali ya Marekani inafurahia kuona mapambano kati ya Russia na Ukraine, kwani kutokana na vita, Marekani itakuwa na kisingizio imara cha kuiwekea vikwazo vikali Russia, na kampuni za silaha za Marekani zitapata faida kubwa zaidi.

Kwa mujibu wa habari mpya zaidi, katibu wa habari wa rais wa Russia Dmitry Peskov alisema, rais Putin yuko tayari kupeleka ujumbe wa Russia kwenda Minsk ili kufanya mazungumzo na ujumbe wa Ukraine.

Jumuiya ya kimataifa inatarajia pande mbili za Russia na Ukraine zijitulie na kujizuia, na kutafuta ufumbuzi wa kiamani kwa njia ya mazungumzo. China siku zote inafuata msimao wa kuheshimu mamlaka na ukamilifu wa ardhi za nchi mbalimbali, na msimamo wa kufuata kanuni za katiba ya Umoja wa Mataifa. China itaendelea kufanya juhudi zake ili kufikisha mazungumzo ya amani, na kuchangia utatuzi wa kisiasa wa suala la Ukraine.