Aliyekuwa naibu katibu mkuu wa UM asema NATO ni chanzo cha mzozo wa Ukraine
2022-02-28 14:11:26| CRI

Aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na mtaalamu wa masuala ya kijamii wa Italia Pino Ariacchi amesema NATO ni chanzo cha mzozo wa Ukraine, na msingi wa utatuzi wake uko mikononi mwa nchi za Ulaya.

Akihojiwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, Pino Ariacchi alisema tangu wakati wa Enzi ya Napoleon, Russia imekuwa ikiuchukulia uvamizi wa magharibi kama tishio kuu. Baada ya Umoja wa Kisoviet kuvunjika, Russia ilihakikishiwa na NATO kwamba haitajipanua kuelekea Ulaya Mashariki, lakini baada ya hapo NATO imeendelea kwenda mashariki na hata kufika kwenye mpaka wa Russia, kitendo ambacho ndio chanzo cha kuilazimisha Russia kufanya operesheni hii ya kijeshi.

Arriach anaona kuwa nchi za Ulaya zinatakiwa kutangaza wazi kuwa NATO haitaivuta Ukraine kujiunga nayo, na makubaliano hayo yasainiwe kwa maandishi, hapo ndio mzozo huo utamalizika.