Putin aviweka tayari vikosi vya matishio ya kimkakati kwa jukumu la kupambana
2022-02-28 14:07:14| CRI

Putin aviweka tayari vikosi vya matishio ya kimkakati kwa jukumu la kupambana_fororder_4

Rais wa Russia Vladmir Putin ameamuru vikosi vya matishio ya kimkakati kuwekwa tayari kwa jukumu la kupambana kwenye mkutano wa Jumamosi na maafisa wakuu wa ulinzi.

Kwenye mkutano na Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu na Mnadhimu Mkuu wa vikosi vya Jeshi la Russia Valery Gerasimov, Putin amesema maafisa waandamizi wa nchi wanachama wa NATO wametoa “taarifa kali” dhidi ya Russia. Amebainisha kuwa nchi za magharibi zinalazimisha vikwazo haramu dhidi ya uchumi wa Russia.

Uamuzi wa kuweka vikosi vya kuzuia mashambulizi umekuja wakati Russia inafanya operesheni maalumu ya kijeshi nchini Ukraine tangu Alhamis. Kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Russia Igor Konashenkov, vikosi vya Russia vimeharibu vifaa vya miundombinu ya kijeshi ya Ukraine vipatavyo 975, na kwa sasa Russia imezingira miji kadhaa mashariki na kusini mwa Ukraine.